Mpanda FM

Recent posts

6 September 2023, 10:10 am

NIshati ya Mafuta Yawa Kikwazo cha Uchumi

MPANDA Nishati ya mafuta ya petrol imetajwa kuwa ni Moja ya sababu inayorudisha nyuma uchumi katika halmashauri ya manispaa ya mpanda mkoani hapa. Wakizungumza na Mpanda redio FM watumiaji wa vyombo vya moto wamesema kuwa wamekuwa wakitumia muda Mwingi kupanga…

4 September 2023, 9:46 am

Madiwani Tanganyika waomba mafunzo ya hewa ya Ukaa

TANGANYIKA Ili Kuitambua biashara ya hewa ya ukaa Madiwani wilaya ya Tanganyika wameitaka Halmashauri hiyo kuwapa madiwani Mafunzo ya biashara ya hewa ya ukaa. Wakizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka Wamesema katika vikao…

4 September 2023, 9:44 am

Watoto Wawili Familia Moja Wafariki kwa Ajali ya Moto

KATAVI. Watoto wawili wa familia moja Florida Froline (3) na Ferisian Froline (3) wamefariki dunia Baada ya nyumba waliokuwemo kuungua Moto mtaa wa Tulieni kata ya Nsemulwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi. Shuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa watoto hao…

30 August 2023, 10:07 am

KKKT wamuaga Ambele Mwaipopo

MPANDA Idara ya wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Jimbo la Katavi wamefanya hafla ya kumuaga Askofu wa Dayosisi ya ziwa Tanganyika Ambele Mwaipopo ambaye anakaribia kumaliza muda wake. Awali akisoma taarifa Mwenyekiti wa Idara ya wanawake…

30 August 2023, 10:03 am

Madiwani Tanganyika wadai uchunguzi fedha za ndani

TANGANYIKA Madiwani wilayani Tanganyika wametaka kufanyika kwa ukaguzi wa ndani wa fedha za mapato ya ndani kutokana na fedha kuwepo lakini kushindwa kupelekwa kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanza kutekelezwa na wananchi. Wakizungumza katika kikao cha robo ya nne ya mwaka…

29 August 2023, 10:12 am

Mpanda Girls Wasisitizwa Kusoma

MPANDA Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mpanda wamesisitizwa kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao. Msisitizo huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ziwa Tanganyika (Rukwa/Katavi)…

29 August 2023, 10:05 am

Kizungumkuti Barabara ya Kabungu – Karema

TANGANYIKA. Baadhi ya Wananchi Mkoani Katavi wanaotumia Barabara ya Kabungu kwenda Karema wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara hiyo na kuitaka serikali kuifanyia matengenezo kwa kiwango cha lami. Wakizungumza na mpanda redio fm kwa nyakati tofauti wananchi hao wameleeza kuwa…

25 August 2023, 10:25 am

TAKUKURU Katavi yawafikisha 7 mahakamani kwa wizi wa bilioni 1.2

KATAVI Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Katavi imewafikisha mahakamani watumishi wa serikali 7 kwa makosa matatu ikiwemo wizi wa fedha zaidi ya bilioni 1.2. Kelvin Mwaja ni mwanasheria kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na…

24 August 2023, 8:39 am

Wakulima Kasokola walizwa na mifugo

MPANDA Baadhi ya wakulima katika kata ya Kasokola halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia wafugaji kulisha mifugo kwenye mazao yao hali ambayo inawarudisha nyuma kiuchumi. Wamebainisha hayo katika mkutano wa hadhara mbele ya mkuu wa wilaya ya Mpanda…

20 August 2023, 3:06 pm

Eden yafutwa machozi kilio cha maji

MPANDA Wananchi wa mtaa wa Edeni kata ya Misukumilo halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamemshuru Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi kwa kuwapambania haraka kupata huduma ya maji safi na salama. Hayo yanajiri kufuatia ziara ya…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.