Mpanda FM

Recent posts

25 November 2022, 4:55 am

Zaidi ya Bilioni 17 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabar

KATAVI Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 17.254 kwaajili ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania Tanroads mkoa wa Katavi Injinia Martin Mwakabende amesema mkoa…

23 November 2022, 6:38 pm

Wafugaji wametakiwa kuondoa mifugo yao katikati ya mji

MPANDA Wafugaji kata ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuondoa mifugo yao na kufugia nje ya mji. Katazo hilo limetolewa na Afisa mtendaji wa kata ya Kashaulili Merry Ngomarufu ambapo amesema wafugaji wote wenye mifugo iliyopo katika kata…

23 November 2022, 5:47 pm

Wafanyabiashara wametakiwa kulipa Ushuru

MPANDA Wafanyabiashara Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kutoa ushuru kikamilifu,ili fedha hizo ziweze kusaidia kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwamo ya elimu na afya. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sofia Kumbuli ambapo amesema kuwa swala…

3 November 2022, 5:58 am

Wanawake Mkoani Katavi Wameeleza Walivyonufaika na Wiki ya Mwanakatavi

KATAVI Baadhi ya wanawake wajasiliamali mkoani Katavi wameeleza namna ambavyo wamenufaika na maonesho ya wiki ya Mwanakatavi yanayolenga kuhamasisha kilimo na Utalii. Wakizungumza wakati wa maonesho hayo wajasiliamali hao wamesema maonesho hayo licha ya kuwanufaisha kibiashara pia wanapata nafasi ya…

3 November 2022, 5:48 am

Anusurika Kifo Baada ya Kuchomwa Kisu na Mumewe (Diwani)

KATAVI Mwanamke anaefahamika kwa majina ya Restuta Januari (Miaka 41) mkazi wa Kata ya Itenka Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi amenusurika kifo baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili wake na anae tajwa kuwa ni…

3 November 2022, 5:29 am

Wananchi wilaya ya Tanganyika Wajitokeza Kupata Chanjo ya Uviko-19

KATAVI Baadhi  ya wananchi  wa Luhafe wilayani Tanganyika wamejitokeza kupata chanjo ya uviko 19 kijijini hapo, inayoratibiwa na taasisi ya Benjamini Mkapa. Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi waliopata chanjo ya Uviko 19, wameishukuru serikali pamoja na wadau kwa…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.