Mpanda FM

Recent posts

15 December 2022, 10:17 am

Majengo mapya kujengwa katika makao makuu ya tarafa Tanganyika

TANGANYIKA Katika kuimarisha huduma za kimahakama mkoani Katavi Serikali imejipanga kujenga majengo mapya katika makao makuu ya tarafa zote wilayani Tanganyika. Hayo yamesemwa na naibu waziri wa katiba na sheria Geofrey Pinda wakati wa ziara ya waziri Mkuu Kassim Majaliwa…

13 December 2022, 9:23 am

Jamila Yusuph aiagiza Ruwasa kukamilisha mradi wa maji Mwamkulu.

MPANDA Mamlaka ya maji manispaa ya mpanda Ruwasa imeagizwa kuhakikisha mradi wa maji katika kata ya mwamkulu unakamilika ili kupunguza adha kwa wananchi. Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph wakati akifanya ziara ya ukaguzi wa…

10 December 2022, 4:36 am

Miaka 61 ya Uhuru wananchi wametakiwa kuunga mkono jitihada za vingozi

TANGANYIKA. Katika kuazimisha miaka 61 ya uhuru wa Tanzania bara wananchi wametakiwa kuziunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na viongozi ikiwa ni sehemu ya kumuenzi mwasisi baba wa taifa mwalimu Julius kambarage nyerere. Kauli hiyo imetolewa na mgeni rasmi ambae ni…

8 December 2022, 5:39 pm

Asilimia 88 ya kaya Mpanda zinatumia vyoo Bora.

MPANDA Asilimia 88 ya kaya katika manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatumia vyoo bora huku asilimia 12 za kaya zilizobaki hazina vyoo bora kutokana na kuwa na hali duni ya Maisha. Akizungumza na Mpanda radio FM afisa afya Manispaa ya…

8 December 2022, 5:33 pm

Bei za mafuta zapokelewa Kwa mikono miwili Katavi

MPANDA Madereva wa vyombo vya moto Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani katavi wametoa maoni yao juu ya mwenendo wa kushuka na kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol na dizel. Wakizungumza na Mpanda Radio fm kwa nyakati tofauti madereva…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.