Mpanda FM

Recent posts

10 April 2023, 4:54 pm

Wananchi Kayenze Walia na TARURA

KATAVI Wananchi wa Kayenze Kata ya Katuma Halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi wamewaomba Wakala wa barabara Vijijini TARURA kurekebisha Barabara ya Sibwesa Katuma inayopita katika eneo lao. Wameiambia Mpanda Radio kuwa wanapata adha ya usafiri na kushindwa kufanya baadhi ya…

8 April 2023, 9:43 am

Mrindoko Apiga Marufuku Watoto Kupelekwa Kumbi za Sherehe Pasaka

KATAVI Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amepiga marufuku Watoto kupelekwa kwenye kumbi za sherehe katika sikukuu ya pasaka. Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake amewataka wananchi kusheherekea sikukuu ya Pasaka kwa upendo na amani na kuhakikisha…

7 April 2023, 7:10 am

Watu 5 Katavi Wakamatwa na Kilo 4 na Kete 209 za Bangi

MPANDA Jeshi la polisi mkoa wa katavi limefanikiwa kuwakamata watu watano wakiwa na kilo nne na kete mia mbili na tisa za madawa ya kulevya aina ya bangi. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa…

7 April 2023, 7:04 am

Wananchi Konamnyagala Wapongeza Jitihada za Kamati ya Shule

KATAVI Wananchi wa Kona ya Mnyagala Kijiji cha Ikaka kata ya Mnyagala Halmashauri ya Tanganyika mkoani katavi wamepongeza Jitihada za Kamati ya Shule katika usimamiaji wa upatikanaji wa Chakula shuleni hapo. Wakizungumza na kituo hiki wamesema kuwa wameitikia Wito wa…

6 April 2023, 9:57 am

Mkazi wa Ibindi Ajinyonga Nyumbani Kwake

KATAVI Mtu mmoja anayefamika kwa jina la Aden Mwakipesile mwenye umri wa miaka 49 mkazi wa kijiji cha Ibindi wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi amekutwa amefariki kwa kujinyonga nyumbani kwake usiku wa kuamkia April 4. Mke wa marehemu Letisia Deus…

6 April 2023, 9:18 am

Kamati ya PETS Yabaini Madudu Shule za Msingi Nsimbo

NSIMBO Kamati ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma katika shule za msingi (PETS) halmashauri ya Nsimbo imebaini uwepo wa uchakavu wa miundombinu,ukosefu wa vyoo mashuleni na uhaba wa walimu. Akisoma taarifa ya Awali wakati akiwasilisha taarifa ya Mrejesho…

6 April 2023, 8:46 am

Serikali Kutatua Mgogoro wa Kagera Group Dhidi ya Wanakijiji Dirifu

MPANDA Serikali imehaidi kutatua mgogoro uliopo kati ya bodi ya kagera group na wanakijiji wa dirifu kata ya magamba ,manispaa ya mpanda mkoani katavi. Hayo yamesemwa na katibu tawala wa manispaa ya Mpanda Kenneth Pesambili akimwakilisha mkuu wa wilaya ya…

6 April 2023, 8:36 am

Kamati ya Shule za Msingi Imetakiwa Kufatilia Miradi Katika Shule za Msingi

MPANDA Kamati za shule za msingi katika halmashuri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi zimetakiwa kuhakikisha zinafuatilia miradi inayofanyika katika shule za msingi. Hayo yamezungumzwa na kaimu afsa elimu msingi wa halmashuri ya manispaa ya Mpanda Victor Mwakajumlwa katika semina…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.