Mpanda FM

Recent posts

12 September 2023, 7:27 am

Waandishi wa habari nyanda za juu kusini wanufaika na mafunzo ya Tadio

Mafunzo haya yatawasaidia waandishi wa habari kuwa na uelewa zaidi kidigital kwa kuchapisha Habari ,Makala  na kufikisha elimu mbalimmbali kupitia radio tadio Na Anna Millanzi – Mbeya Waandishi wa Habari wa radio jamii nyanda za juu kusini wamepatiwa mafunzo ili…

11 September 2023, 9:55 am

Watoto wawili wa familia moja  wafariki kwa ajali ya moto Katavi

Katika eneo la tukio kimekutwa kiberiti ambacho kinadhaniwa kuachwa na mtu . Na William Liwali-Katavi Watoto wawili wa familia moja  Florida Froline   na Ferisian Froline wenye umri wa miaka mitatu wamefariki dunia  baada ya nyumba yao kuungua  moto mtaa wa…

11 September 2023, 8:27 am

Wakulima waaswa kuchukua mbolea mapema

MPANDAWakulima halmashauri ya Mpanda mkoani Katavi wameshauriwa kuchukua mbolea mapema ili kuepukana na changamoto ambazo zilitokea katika msimu wa kilimo uliopita. Afisa kilimo Manispaa ya Mpanda Gwalusajo Kapande amesema kuwa zoezi la ununuzi wa mbolea limeanza Septemba 1, 2023 hivyo…

11 September 2023, 7:54 am

Wanafunzi 6000 Mpanda wataraji kuhitimu darasa la saba

MPANDA Zaidi ya Wanafunzi 6000 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba Manispaa ya Mpanda katika Mtihani Unaotarajiwa kufanyika Sept 13 na 14 mwaka 2023. Akizungumza na Mpanda Radio fm Afisa Elimu Shule za Msingi Manispaa ya Mpanda Godfrey…

6 September 2023, 10:18 am

Wanawake Waaswa Kuwa Wabunifu

MPANDA Baadhi ya wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametoa maoni mseto juu ya namna gani wanawake wanaweza kuchangamkia fursa za uvumbuzi na ubunifu katika kujitafutia kipato na kuondokana na umaskini. Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm kwa…

6 September 2023, 10:15 am

Mrindoko Aahidi Malipo ya Tumbaku

KATAVI Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewahakikishia malipo zaidi ya Dola Milioni 2.5 wakulima wa zao la Tumbaku katika msimu wa kilimo 2022/2023 wa Amcos 6 zilizoingia Mkataba wa ununuzi wa Tumbaku na Kampuni ya Mkwawa Leaf LTD.…

6 September 2023, 10:10 am

NIshati ya Mafuta Yawa Kikwazo cha Uchumi

MPANDA Nishati ya mafuta ya petrol imetajwa kuwa ni Moja ya sababu inayorudisha nyuma uchumi katika halmashauri ya manispaa ya mpanda mkoani hapa. Wakizungumza na Mpanda redio FM watumiaji wa vyombo vya moto wamesema kuwa wamekuwa wakitumia muda Mwingi kupanga…

4 September 2023, 9:46 am

Madiwani Tanganyika waomba mafunzo ya hewa ya Ukaa

TANGANYIKA Ili Kuitambua biashara ya hewa ya ukaa Madiwani wilaya ya Tanganyika wameitaka Halmashauri hiyo kuwapa madiwani Mafunzo ya biashara ya hewa ya ukaa. Wakizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka Wamesema katika vikao…

4 September 2023, 9:44 am

Watoto Wawili Familia Moja Wafariki kwa Ajali ya Moto

KATAVI. Watoto wawili wa familia moja Florida Froline (3) na Ferisian Froline (3) wamefariki dunia Baada ya nyumba waliokuwemo kuungua Moto mtaa wa Tulieni kata ya Nsemulwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi. Shuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa watoto hao…

30 August 2023, 10:07 am

KKKT wamuaga Ambele Mwaipopo

MPANDA Idara ya wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Jimbo la Katavi wamefanya hafla ya kumuaga Askofu wa Dayosisi ya ziwa Tanganyika Ambele Mwaipopo ambaye anakaribia kumaliza muda wake. Awali akisoma taarifa Mwenyekiti wa Idara ya wanawake…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.