Mpanda FM

Recent posts

16 November 2024, 6:59 pm

Katavi: Wanufaika wa TASAF wapongezwa kwa kazi wanazozifanya

“Wanufaka wa mradi wa TASAF wanafanya kazi kwa bidii kwa kukarabati miundombinu ikiwemo ya barabara” Na Samwel Mbugi -Katavi Naibu Waziri ofisi ya Rais Utumishi na utawala bora Deus Sangu ambae ni Mbunge wa jimbo la Kwela mkoa wa Rukwa…

16 November 2024, 6:02 pm

Wakuu wa idara Tanganyika watakiwa kutatua changamoto

“acheni kukaa ofisini nendeni mkawahudumie wananchi“ Na Anna Milanzi -Katavi Mkuu wa wilaya ya Tanganyika ameagiza viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo kusimamia ipasavyo nakuwataka maafisa ugani kuwatembelea wakulima katika mashamba yao . Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa…

15 November 2024, 8:20 pm

Kivuko chenye thamani ya Tshs milioni 9.8 chakabidhiwa kwa serikali

“Baada ya kuombwa na wananchi kusaidia kutengeneza kivuko hicho alifuata taratibu zote na kupata kibali TARURA.“ Na Samwel Mbugi -Katavi Mdau wa maendeleo mkoa wa Katavi Injinia Ismail Nassor Ismail amekabidhi kivuko kwa serikali Chenye thamani ya shilingi milioni tisa…

14 November 2024, 12:25 pm

RC Katavi awataka wananchi kujitokeza wakati wa kampeni, upigaji wa kura

 Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na wananchi.picha na Lilian Vicent “amewaomba kujitokeza kushiriki kampeni  zitakapoanza ili  kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi bora.“ Na Lilian Vicent -Katavi Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wananchi wote…

14 November 2024, 12:12 pm

Katavi: Bilion 2.9 kulipa fidia wananchi wanaopisha mradi wa miji 28

Baadhi ya Wananchi ambao wametoa maeneo yao na kupisha mradi wa miji 28 .picha na Lilian Vicent “ametaka fedha hizo zitumike vizuri sio kuleta  migogoro ndani ya familia.” Na Lilian Vicent-Katavi Wananchi 568 wanaopisha ujenzi wa mradi wa miji 28…

12 November 2024, 12:47 pm

RC Katavi atoa wito kwa wadau wa uchaguzi kuzingatia sheria

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko.picha na Rachel Ezekia “amewakumbusha wananchi kujitokeza kwenye vituo walivyojiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.“  Na Ben Gadau -Katavi Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,ametoa wito kwa wadau wa uchaguzi…

8 November 2024, 3:58 pm

Katavi:Vijana wahimizwa kupima afya mara kwa mara

picha na mtandao ” vijana wa kiume hawajitokezi katika suala la upimaji afya zao ikilinganishwa na vijana wa kike.” Na Rhoda Elias -Katavi Vijana  manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuwa na desturi ya kujitokeza ili kupima afya zao mara…

8 November 2024, 3:32 pm

Katavi :vishikwambi 23 kuongeza ufanisi wa kazi kwa maafisa ugani

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry wa kwanza kulia akikabidhi kishikwambia kwa afisa ugani .picha na John Benjamin Na John Benjamini-Katavi Vishikwambi 23 vimegawiwa kwa Maafisa Ugani Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi…

8 November 2024, 3:17 pm

Katavi:mtendaji kata apewa adhabu ya kukatwa mshahara kwa kipindi cha miaka 3

kikao cha baraza la madiwani Nsimbo.picha na Rachel Ezekia “Mtendaji huyo licha ya kuitwa mara kadhaa na mwajiri wake na kuonywa bado aliendelea kutozingatia maagizo ndipo ilipoundwa tume ya uchunguzi kisha kurudisha majibu Hatimaemaamuzi yamefanyika.“ Na Rchel Ezekia -katavi Baraza…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.