Mpanda FM
Mpanda FM
4 December 2025, 9:03 am
“Wafugaji hawaelewi ukimwambia leo kesho anarudia tena” Na Restuta Nyondo Ongezeko la mifugo katika eneo la Kidakio cha Mto Katuma imetajwa kuwa chanzo cha uharibifu wa vyanzo vya maji mkoani Katavi. Felista Madeleke mjumbe wa kamati mto Katuma amesema kuwa…
3 December 2025, 3:56 pm
“Wawe makini katika kuangalia tabia na marafiki walionao” Na Anna Mhina Vijana mkoani Katavi wametakiwa kuwa makini katika kuchagua marafiki wa kuambatana nao ili kuweza kuepuka kujiunga na makundi mabaya yatakayohatarisha maisha yao. Akizungumza na Mpanda radio FM afisa maendeleo…
2 December 2025, 3:23 pm
“Tunawahakikishia tunawalink na taasisi mbalimbali za kifedha” Na Anna Milanzi Vijana kutoka katika kikundi cha kijana jitambue kilichopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamehamasika kulima zao la alizeti kutokana na zao hilo kuwa na thamani . Hayo yamejiri mara baada…
27 November 2025, 11:58 am
“Tunaihamasisha jamii itunze vyanzo vya maji kwa sababu ni muhimu” Na Leah Kamala Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameeleza madhara katika mazingira endapo vyanzo vya maji vitaharibiwa. Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa…
27 November 2025, 9:26 am
Na Anna Mhina Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kutoa elimu ya masuala ya uzazi wa mpango ili waweze kuepukana na mimba zisizotarajiwa. Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa wanapewa dawa za…
26 November 2025, 10:51 am
“Mvua zinazoendelea kunyesha zinaleta madhara makububwa “ Na Samwel Mbugi Wafanyabiashara wa soko la Mpanda hotel wameiomba serikali kushughulikia changamoto ya mifereji ya kupitishia maji hususani kipindi hiki cha mvua zilizoanza kunyesha ili isije kuleta madhara ya magojwa ya mlipuko.…
26 November 2025, 10:30 am
“Hakikisheni mnakuwa wabunifu katika kutoa huduma” Na Restuta Nyondo Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameziagiza taasisi zote za umma kutoa huduma bora na ufanisi kwa wananchi na kuhakikisha wanakua wabunifu katika utoaji wa huduma bila visingizio. Ameyasema…
25 November 2025, 7:01 pm
“Sisi tunathamini mchango mnapokuwa na jambo lolote mtufikie” Na John Benjamin Wananchi wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wameaswa kudumisha amani na mshikamano utakaokuwa nyenzo muhimu wa kufanya shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa masirahi taifa kwa ujumla.…
22 November 2025, 11:18 am
“Nataka hizo wiki mbili nione kazi ya maana imefanyika” Na Benny Gadau Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa daraja la Mirumba lenye thamani ya zaidi ya billion 6 katika halmashauri ya Mpimbwe mkoani…
22 November 2025, 10:31 am
Waziri Mbarawa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa bandari hiyo. Picha na Samwel Mbugi “Sasa tunajenga meli nne kwa mpigo” Na Samwel Mbugi Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa amelizishwa na utengenezaji wa meli nne zinazotengenezwa bandari ya Karema mkoani…
Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.
Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.
Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.
Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.
