Mpanda FM

Watatu wafariki ajali ya gari Katavi

7 April 2026, 6:22 pm

SACP Kaster Ngonyani kamanda wa polisi Katavi. Picha na Anna Mhina

“Jeshi la polisi linatoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani”

Na Benny Gadau

Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi linatoa taarifa ya tukio la ajali ya gari iliyotokea barabara kuu ya Mpanda – Sumbawanga baada ya kuacha njia na kugonga karavati kisha kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu watu.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba  mnamo tarehe 06.04.2026 majira ya saa 06:45 alfajiri huko katika Kijiji cha Magamba wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi gari namba T 693 DJP aina ya Toyota Succeed mali ya David Thobias (37) ikiendeshwa dereva Kassim Mohamed akiwa abiria wawili ambao hawajatambulika kwa majina wakitokea Mpanda mjini kuelekea Stalike gari hilo liliacha njia na kugonga karavati kisha kuwaka moto na kusababisha vifo vya abiria hao pamoja na dereva.

Sauti ya kamanda

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva kushindwa kulimudu gari lake kisha kuhamia upande wa pili wa barabara na kugonga karavati.

Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi limetoa wito kwa madereva wote kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa kufuata alama za michoro iliyowekwa barabarani na kuchukua tahadhari

Sauti ya kamanda