Mpanda FM

Kupanda bei nishati ya mafuta kilio kwa abiria Katavi

3 April 2026, 7:21 pm

Allen Mwandri afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini mkoa wa Katavi. Picha na John Benjamin

“Kwanza ni marufuku msafirishaji yeyote kupandisha nauli”

Na John Benjamin

Mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini [Latra] mkoa wa Katavi imepiga marukufu mawakala wa usafirishaji kupandisha bei ya nauli kiholela kwa abiria mara baada ya kupanda kwa  bei ya nishari ya mafuta.

Hayo yamejiri kufuatia maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Katavi ambapo afisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri ardhini mkoa wa Katavi Latra Allen Mwandri amesema kuwa ni kosa kisheria mtu yeyote kupandisha bei  ya nauli bila ya maelekezo ya serikali huku akiwataka kuwa watulivu katika kipindi hiki serikali ikiwa inapitia upya na kuja na maelekezo.

Sauti ya Allen Mwandri

Kwa upande wao baadhi ya mawakala usafirishaji katika stendi ya Mizengo Pinda wamesema kuwa kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta wamekuwa wakipata hasara na kuiomba serikali  kupitia kwa kina na kutatua changamoto hiyo.

Sauti za mawakala

Nao baadhi ya abiria katika stendi ya Mizengo Pinda wamesema kuwa nauli imepanda hali ambayo inawagharimu na kushindwa kumudu bei hiyo na kuiomba serikali kuwasaidia kwa kulitazama jambo hilo ili kuondokana na adha hiyo.

Sauti za abiria

Hivi karibuni serikali nchini Tanzania ilitangaza bei mpya ya nishati ya mafuta kwa mwezi huu wa nne ikiwa na ongezeko.