Mpanda FM

Kakulukulu: Tuendelee kuitunza amani ya nchi yetu

23 March 2026, 3:19 pm

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi Nassoro Kakulukulu. Picha na Samwel Mbugi

“Lengo letu ni kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo katika mkoa wetu”

Na Samwel Mbugi

Sheikh mkuu wa mkoa wa Katavi Nassoro Kakulukulu ameendelea kuhimiza amani na mashirikiano baina ya dini zote katika kuhakikisha wanaihubili amani ya nchi ya Tanzania.

Akizungumza katika baraza la idd lililofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda amesema  lengo la mashirikiano na taasisi za dini ni kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kutawala kwa mkoa wa Katavi na Tanzania kwa ujumla.

Sauti ya sheikh mkuu

Kwa upande wa mchungaji Enduru Masumo ametoa shukurani kwa umoja  na msikamano kwa sheikh mkuu kwa kuendelea kuonyesha ushirikiano na dini zote jambo ambalo ameahidi kuonesha mshikamano huo.

Sauti ya mchungaji

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrondoko amesema wanatambua mchango unaotolewa na taasisi za dini katika kuwahudumia wananchi.

Sauti ya mkuu wa wilaya

Hata hivyo Jamilia ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa katavi kuendelea kuwa na mshikamano katika kuhakikisha amani inaendelea kuwepo.