Mpanda FM
Mpanda FM
20 March 2026, 5:37 pm

“Amekutwa amefariki dunia kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili “
Na Ben Gadau -Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika jina moja la Haidari anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 mwalimu wa shule ya msingi Nguvumali amekutwa amefariki dunia kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili katika Mtaa wa Mkwajuni kata ya Mwamkulu Manispaa ya Mpanda.
Wakizungumza kwa njia ya simu na Mpanda Redio FM baadhi ya wananchi wa mtaa huo wameonesha kusikitishwa na tukio hilo huku wakiomba vyombo vya dola kuhakikisha wanawachukulia hatua wote walio husika, ili kukomesha matukio ya aina hiyo.
Amosi Mtingwa ni mwenyekiti wa mtaa wa mkwajuni amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akiwaasa wananchi wa mtaa huo kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo.
Jitihada za kulitafuta jeshi la polisi zinaendelea na zikikamilika watatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.