Mpanda FM

Wananchi Mpanda “Bomba likipasuka fursa kwetu”

11 March 2026, 4:37 pm

Mhandisi Philipo Pagati meneja usambazaji maji Mpanda. Picha na Anna Mhina

“Ni kosa kisheria kutotoa taarifa pindi bomba linapopasuka”

Na Anna Mhina

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mpanda hotel uliopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (MUWASA) kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutoa taarifa pindi wanapoona bomba la maji limepasuka.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa ukosefu wa elimu unapelekea mamlaka kupata hasara huku wengine wakichukulia kama fursa ya kupata maji kwa urahisi kutokana na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Sauti za wananchi

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (MUWASA) ambaye pia ni meneja usambazaji maji Mpanda mhandisi Philipo Pagati amesema ni kosa kisheria kwa mwananchi kutotoa taarifa na kueleza mikakati yao kama mamalaka ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu katika kila mtaa.

Sauti ya mhandisi Pagati

Hata hivyo tatizo la ukosefu wa maji safi na salama limekuwa likiwakabili wananchi katika maeneo mbalimbali Katavi ambapo wengine hulazimika kutembea umbali mrefu au hata kununua maji ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku.