Mpanda FM

Mwanakulya “Wanawake chachu ya maendeleo”

6 March 2026, 6:00 pm

Baadhi ya wanawake wa Mpanda katika picha ya pamoja. Picha na Samwel Mbugi

“Msherehekee na kuanzimisha siku ya wanawake duniani”

Na Samwel Mbugi

Wanawake manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutambua na kuthamini mchango wa mwanamke katika jamii.

Akizungumza mbele ya wanawake katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda mgeni rasmi Fedensiana Mwanakulya ambae ni katibu tawala wilaya ya Mpanda akimwakilisha mkuu wa wilaya Jamila Yusuph amesema wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya jamii

Sauti ya katibu tawala

Akisoma tarifa mbele ya mgeni rasmi afisa maendeleo ya Jamii Respista Kalugendo ameainisha shughuli walizozifanya ikiwemo kupanda miti 400 katika shule ya msingi Mkapa pamoja na matendo ya huruma kwa watu wenye mahitaji maalumu.

Sauti ya afisa maendeleo

Ikumbukwe kuwa maadhimisho hayo kila mwaka huwa yanaanza tarehe moja ya mwezi wa tatu na kutamatika tarehe nane ya mwezi wa tatu, na kauli mbiu ya mwaka huu 2026 ni haki na usawa kwa wanawake na wasichana msingi jumuishi kufikia dira 2050.