Mpanda FM

Lyamba sekondari yapokea Kompyuta

6 March 2026, 3:34 pm

Katibu mwenenzi akimkabidhi mwalimu kompyuta hizo. Picha na Betord Chove

“Walitupatia changamoto nyingi”

Na Betord Chove

Katibu mwenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Nsemulwa  wilayani Mpanda mkoani Katavi Geofrey Alfonce Kipeta amekabidhi kompyuta mbili  za  mezani kwa shule ya sekondari Lyamba.

Akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa hivyo, Kipeta amesema amepeleka vifaa hivyo kufuatia ziara  aliyofanya tarehe 3 mwezi wa 2  iliyokua na lengo la kutambua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo.

Sauti ya katibu mwenezi

Awali akisoma risala wakati wa makabidhiano hayo mkuu wa shule ya Sekondari Lyamba Josylin N. Myango  amesema ujio wa kompyuta hizo utakwenda kuongeza ufaulu wa wanafunzi kutokana na  changamoto mbalimbali za vifaa zilizokuepo katika shule hiyo.

Sauti ya mkuu wa shule

 Cyspin Myango mwenyekiti wa bodi ya shule na kaka mkuu wa shule hiyo wakizungumza  kwa niaba ya wazazi na wanafunzi wametoa shukurani kwa mdau huyo wa elimu kwa mchango huo  na kumwomba kutatua changamoto nyingine zinazowakabili ikiwemo Kichapishi.

Sauti ya mwenyekiti wa bodi

 Kwa mujibu wa mkuu wa  shule hiyo , sekondari ya  Lyamba imeanzishwa mwaka 2022  ikiwa na wanafunzi  246 kwa sasa ina wanafunzi 980 huku  wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo madawati, Kichapishi na Kiangazishi.