Mpanda FM
Mpanda FM
5 March 2026, 3:51 pm

“Maelekezo ya serikali ni kupnda miti katika maeneo yetu”
Na Samwel Mbugi
Jumla ya miti 400 ya matunda na kivuli imepandwa na wanawake katika shule ya msingi Mkapa iliyopo manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wakizungumza mara baada ya kupanda miti baadhi ya wanawake waliojitokeza katika zoezi hilo wamesema miti ya matunda inaumhimu kwa ukuaji wa mtoto kwa kupata lishe bora na kusaidia uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika zoezi hilo Anna Shumbi ambae ni mkuu wa idara ya maendeleo mkoa wa Katavi amesema kupanda miti ni maelekezo ya serikali katika kuhakikisha wananchi wanahamasika kupanda miti ya matunda na kivuli.
Hata hivyo shumbi amesema upandaji wa miti ya matunda ni mhimu kwani inaenda sambamba na mkakati wa kukabiliana na changamoto ya lishe kwa mkoa wa Katavi.