Mpanda FM
Mpanda FM
5 March 2026, 2:02 pm

“Niwasihi wananchi wa Mpanda waweze kufika ili watatuliwe migogoro ya ardhi”
Na John Benjamin
Wananchi wilaya ya Mpanda wametakiwa kuchangamkia fursa ya kampeni ya klinki ya Samia iliyolenga kutatua changamoto, migororo na kutoa hati ya ardhi.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusufu wakati wa uzinduzi wa klinki hiyo ambapo amesema kuwa klinki hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kusikiliza na kutatua migogoro ikiwemo kutoa hati za umiliki wa ardhi na kumpunguzia mwananchi kupoteza muda kwenda ofisi za ardhi.
Kwa upande wake Kamishina msaidizi wa ardhi mkoa wa Katavi Chediel Mrutu amesema kuwa mkoa wa Katavi kwa sasa migogoro imekupungua kutokana na namna ambavyo wamekuwa wakitatua migogoro hiyo huku akiongeza kuwa kupitia kampeni hiyo zaidi ya wananchi 80 wamefika na kupatiwa huduma mpaka sasa.
Nao baadhi ya wananchi waliofika katika viwanja hivyo wamepongeza serikali kwa kuwasongezea huduma ambapo wameleeza kuwa huduma hiyo imewapunguzia mizunguko ya kufuatilia na kuwarahisishia kupata hati kwa urahisi zaidi.
Kampeni ya kliniki ya samia imelenga kusikiliza, kutatua na kutoa hati ya umiliki wa ardhi ambapo kilinki hiyo imeanza tarehe 01 na inatarajiwa kukamilika terehe 08 mwezi huu.