Mpanda FM

Shilingi 300 zaleta mjadala baraza la madiwani

2 March 2026, 3:48 pm

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha pili cha baraza. Picha na Samwel Mbugi

“Sasa mimi nisipokuwa na mia tatu ina maana nibaki”

Na Samwel Mbugi

Baraza la madiwani manispaa ya Mpanda mkoani Katavi limepiga marufuku matumizi ya tiketi za mkono zinazotumiwa na maajenti wa stendi ya kuu ya mabasi Mizengo Pinda kutokana na changamoto ya usumbufu wanaopata abiria ndani ya stendi hiyo.

Hayo  yamejiri katika mkutano wa pili wa baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha 2025/2026 uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkurugenzi baada ya madiwani kuhoji kuhusu ushuru wa sh. 300 unaotolewa mlangoni ukiwa na tiketi iliyoandikwa kwa mkono.

Sauti za madiwani

Kupitia kikao hicho mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Haidary Hemed Sumry amekitaka kiti cha mwenyekiti wa kikao hicho ambae ni meya wa manispaa ya Mpanda kutoa msimamo baada ya kuona hakuna sababu za msingi kuwepo kwa tiketi hizo.

Sauti ya mbunge

Mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda Charles Philipo amesema atakaebainika anatoa tiketi ya mkono atachukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho na wengine.

Sauti ya mstahiki meya

Ikumbukwe kuwa mwaka jana mkuu wa mkoa wa Katavi alitembelea stendi hiyo kwajili ya kusikiliza kero za wasafiri na miongoni mwa kero ilikuwa ni hiyo ambayo alitoa maagizo kwa mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda kulifuatilia hilo kama lina umuhimu wa kutozwa abilia sh. 300 pindi anapoingia stendi.