Mpanda FM

Wananchi wachekelea bwawa la Iziwasungu

2 March 2026, 3:28 pm

Balozi Baraka Luvanda akipokea maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Mpimbwe. Picha na Samwel Mbugi

“Mradi huu umetutoa katika shida na masikitiko”

Na Samwel Mbugi

Wananchi wa Kata ya Kansansa  halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele wametoa shukrani kwa serikali kwa kuwawezesha kupata Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania uliowasaidia kuwachimbia bwawa la maji la Iziwasungu katika kuhakikisha wanapapata maendeleo.

Wakizungumza mbele ya Naibu katibu mkuu ofisi ya makamu wa rais mazingira balozi Baraka Luvanda wamesema Bwawa limekuwa msaada kwa wakazi wa eneo hilo kwa wafugaji na uhifadhi wa mazingira.

Sauti za wananchi

Kwa upande wake diwani wa kata ya Majimoto ambae pia ni  mwenyekiti wa halmashauri Silas Robert Ilumba amemuomba naibu katibu mkuu kuwatafutia mwekezaji kwenye mradi wa hewa ukaa.

Sauti ya diwani

Hata hivyo Balozi Naibu katibu mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Baraka Luvanda amesema jambo hilo la halmashauri ya mpimbwe amelichukua na kwenda kulifanyia kazi.

Sauti ya Luvanda

Ziara hiyo imeweza kutembelea miradi mitatu pamoja na kivutio cha maji ya moto, sehemu ambayo wapimbwe hufanya matambiko ya aina mbalimbali kama vile kuondoa mikosi na magonjwa.