Mpanda FM
Mpanda FM
26 February 2026, 3:37 pm

Daraja lililovunjika na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano. Picha na Betord Chove
“Hakuna mtanzania anayeweza kuingia Karema”
Na Betord Chove
Daraja linalounganisha vijiji vya Ikola, Karema na makao makuu ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi limekatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Baadhi ya wananchi wamesema wanalazimika kuvuka mto kwa kutumia mtumbwi, ambao hulipia shilingi 1,000, jambo linaloongeza ugumu wa maisha yao ya kila siku.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya barabara (TANROADS) Mkoa wa Katavi, Mhandisi Albert Laizer, amesema kazi ya kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo tayari imeanza ili usafiri urejee kawaida.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, ameagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kufanya kazi usiku na mchana ili barabara kutoka Tanganyika kuelekea Bandari ya Karema irejee utendaji wake wa kawaida haraka.
Aidha, amemuagiza Kamanda wa Kikosi cha Uokoaji kupeleka boti maalumu kuvusha wananchi salama na kupiga marufuku matumizi ya mitumbwi hatarishi.