Mpanda FM

Wahusika kukiona

25 February 2026, 11:05 am

Nilimtuma mdogo wake hakumkuta,tukaenda wote kumtafuta hadi usiku wa saa sita hatukufanikiwa kumuona basi tukafunga mlango tukalala

Na Anna Milanzi -Katavi

Kufuatia mauaji ya  Irene Yosia binti mwenye  umri wa miaka 16 mkazi wa mtaa wa tulieni manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, viongozi wa mtaa na kata ya Nsemulwa wamekemei vitendo hivyo viovu.

Mwili wa binti huyo umehifadhiwa katika makazi yake ya milele siku ya jumanne February 24, 2026 katika makaburi yaliyopo kwenye mtaa huo wa tulieni.

Mara baada ya mazishi mwenyekiti wa mtaa huo Hussein Kasomela amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kubaini wahamiaji katika mtaa huo.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa tulieni

Mtendaji wa mtaa  tulieni Prosper Mwesiga amewataka wananchi wa mtaa huo kulinda amani na kujikita katika utafutaji na kila mmoja ajiandikishe katika daftari la wakazi.

Sauti ya mtendaji wa mtaa tulieni

Diwani wa Kata ya Nsemulwa Alex Ngereza ametoa pole kwa familia iliyofikwa na msiba huo na kusema kuwa wanaofanya vitendo hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao

Baba mzazi ameeleza kuwa simu ya binti yake huyo ilikuwa inaita kila wakati usiku wa saa tatu na alikuwa haipokei hadi alipotoka nje ya nyumba yao na hakurejea tena ,wakamtafuta bila mafanikio hadi asubuhi alipoitwa na kuoneshwa mwili wa binti yake ukiwa katika shimo jirani na nyumba yao.