Mpanda FM
Mpanda FM
24 February 2026, 7:05 pm

Baadhi ya viongozi katikati ni mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Haidary Sumry. Picha na Samwel Mbugi
“Tunaishukuru serikali tumepokea vifaa tiba”
Na Samwel Mbugi
Hospitali ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imepokea vifaa tiba 46 kutoka serikali ya awamu ya sita vyenye thamani ya shilingi million 372 ili kuboresha huduma za mama na mtoto ikiwemo mashine ya ultra sound.
Akizungumza mbele ya viongozi wa serikali mganga mkuu wa hospitali Dr. Paul Swakala ametoa shukrani kwa serikali ya muungano wa Tanzania kwa kuwawezesha kupata vifaa tiba ambavyo vitapunguza changamoto zinazowakumba katika majukumu yao.
Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Gwalusajo Kapande amesema vifaa hivyo vitaboresha huduma za afya kwa wananchi, na ameahidi kuvitunza ili viendelee kutumika kwa wagonjwa.
Hata hivyo mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Haidary Hemed Sumry ambae amekabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya serikali amesema kuwa vifaa hivyo vitakuwa kichocheo cha kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa manispaa ya Mpanda.