Mpanda FM

Halmashauri ya manispaa Mpanda yatenga billion 35.2

23 February 2026, 7:05 pm

Katikati ni mstahiki meya wa halmashauri ya Mpanda. Picha na Samwel Mbugi

“Hatuwezi kutengeneza miradi kama hatukusanyi mapato”

Na Samwel Mbugi

Baraza la madiwani halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi imepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti zaidi ya shilingi billioni 35 kwa mwaka wa fedha 2026/2027

Akisoma taarifa mbele ya madiwani kwa niaba ya mkurugenzi  wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli,  afisa mipango Leonard Kilamhama amesema kati ya fedha hizo mapato ya ndani itakuwa billion 7.8 ambapo ruzuku ya maendeleo kutoka kwa wafadhili ni bilioni 2.6.

Sauti ya afisa mipango

Kwa upande wake meya wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Charles Philipo kwa niaba ya baraza la madiwani amewataka watumishi wa umma wanaohusika na ukusanyaji wa mapato kuwa waadilifu  na kuongeza kasi ili kutimiza lengo la kukamilisha miradi iliyopo kupitia bajeti hiyo.

Sauti ya mstahiki meya

Hata hivyo mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Katavi ambae ni afisa serikali za mitaa Gwamaka Owden amempongeza meya pamoja na wakuu wa idara kwa kuongeza vyazo vya ukusanyaji wa mapato ikilinganishwa na bajeti iliyopita.

Sauti ya Gwamaka

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni waziri mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akiwa katika ziara zake alitoa maagizo ya kutenga bajeti itakayoenda kukidhi mahitaji ya wananchi kwa halmashauri zote nchini.