Mpanda FM

Miradi ya ujenzi, michezo yamvuta diwani

20 February 2026, 5:44 pm

Diwani wa Kata ya Ibindi akiwa anazungumza na walimu na wanafunzi katika shule ya msingi muungano.picha na Ben Gadau

ameomba kuharakishwa kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo ili kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wa eneo hilo.

Na Ben Gadau- Katavi

Diwani wa Kata ya Ibindi Mdakuni Matongo ametembelea na kukagua  ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi muungano halmashauri ya Nsimbo iliyopo wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi.

Akizungumza katika eneo hilo, Mdakuni ameomba kuharakishwa kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo ili kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wa eneo hilo.

Sauti ya diwani wa Kata ya Ibindi
Diwani kata ya Ibindi.picha na Ben Gadau

 
Akiwa katika shule ya msingi Muungano, Mdakuni ametoa zawadi ya mipira pamoja na vifaa vingine vya michezo akisema kuwa hiyo itawasaidia wanafuzi hao kufanya mazoezi ili kujijenga na kuwa na afya bora

Sauti ya diwani pamoja na shukrani za walimu na wanafunzi