Mpanda FM
Mpanda FM
20 February 2026, 4:42 pm

“soko hilo linakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundo mbinu hali ambayo inatishia usalama wa bidhaa za wafanya biashara hususani nyakati za usiku.“
Na John Benjamin -Katavi
Wafanyabiashara wa soko kubwa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamewaombea msamaha wa kutosimamishwa kazi maafisa biashara,Manunuzi na Mhandisi wa manispaa hiyo kwa kutofanya ukarabati wa soko hilo.
Hayo yamejiri katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko alipotembelea soko hilo na kubaini kutotekelezwa kwa maagizo yake aliyoyatoa mnamo Disemba 10,2025 juu ya ukarabati wa miundombinu ya soko hilo hususani uchakavu wa paa ambayo imekuwa changamoto katika msimu huu wa masika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko kubwa Bahati Issa Ndagije amesema soko hilo linakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundo mbinu hali ambayo inatishia usalama wa bidhaa za wafanya biashara hususani nyakati za usiku.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo wamesema kuwa wamewaombea msamaha maafisa hao ili kuwapa muda wa kujitafakari na kurekebisha makosa yao tofauti na kusimamishwa kazi huenda changamoto hizo zisitatuliwe kwa wakati.
Kufuatia ziara hiyo Mrindoko ametoa mwezi mmoja kuhakikisha wanatekeleza ukarabati wa miundombinu ya soko hilo.