Mpanda FM

Avunjwa mguu na mke wake, fedha chanzo

19 February 2026, 4:06 pm

Picha na Mwananchi

“Nilifuatwa na mtoto kwa ajili ya kwenda kumsaidia baba yake ambaye alikuwa anavuja damu na baada ya kufika nilimkuta kaka amevunjwa Mguu.”

Na Samwel Mbugi- Katavi

Mwanaume mmoja mwenye umri kati 40 – 45 ambaye jina lake limehifadhiwa amepigwa na kuvunjwa mguu na mke wake baada ya kutokea ugomvi baina yao.

Akizungumza na Mpanda Redio FM dada wa majeruhi amesema kuwa alifuatwa na mtoto kwa ajili ya kwenda kumsaidia baba yake ambaye alikuwa anavuja damu na baada ya kufika alikuta kaka yake amevunjwa Mguu.

Sauti ya Dada wa majeruhi

Hata hivyo Mpanda Redio FM haikuishia hapo imefanya jitihada za kumtafuta mwenyekiti wa mtaa wa Kivukoni Jastine Michael ambaye nae amesema alipigiwa simu na dada wa mgonjwa akihitaji afike eneo la tukio na baada ya kufika alikuta damu zikivuja na kuamua kuchukua hatua ya kumpeleka hospital kwa ajili ya matibabu.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Kivukoni Jastine Michael

Hata hivyo Majeruhi ambaye alipigwa na mke wake hakuwa tayari kuzunguzia tukio hilo ambapo amesema atalizungumzia baada ya wiki mbili kupita.