Mpanda FM
Mpanda FM
18 February 2026, 11:34 am

“kupitia mafunzo hayo wanaamini kuendelea kuwapata wadau zaidi ambao watakuwa mabalozi juu ya uhifadhi wa mazingira katika utunzaji wa hewa ya carbon kwenye maeneo yao.“
Na Ben Gadau -Katavi
Shirika la IUCN International Union For Conservation Of Nature limetoa mafunzo ya uhifadhi wa mazingira kwa wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Katavi.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo Scolastika Dickson Program officer kutoka katika shirika hilo amesema kuwa kupitia mafunzo hayo wanaamini kuendelea kuwapata wadau zaidi ambao watakuwa mabalozi juu ya uhifadhi wa mazingira katika utunzaji wa hewa ya carbon kwenye maeneo yao.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamelishuruku shirika hilo, huku wakisema kuwa kupitia elimu hiyo itawasaidia kuhakikisha utunzaji wa mazingira unafanyika kwa tija ili kuleta maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Mafunzo hayo yameeandaliwa na shirika la International Union For Conservation Of Nature IUCN, na yamefanyika katika ukumbi wa St Mathias Manispaa ya Mpanda ikijumuisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Katavi.