Mpanda FM
Mpanda FM
12 February 2026, 5:55 pm

Dr. Juma Zuberi Homera waziri wa katiba na sheria. Picha na Restuta Nyondo
” Utekelezaji wa huduma hii uanze mikoa yote ya Tanzania bara”
Na Restuta Nyondo
Waziri wa katiba na sheria dkt .Juma Zuberi Homera ameagiza wakala wa usajili, ufilisi na udhamini RITA kuanza utekelezaji wa mfumo wa mobile kliniki nchini ili kurahisisha upatikanaji huduma kwa wadau.
Ameyazungumza hayo wakati akizindua mkutano wa wajumbe wa bodi za wadhamini wa taasisi zilizopo katika mikoa ya Katavi, Kigoma, Tabora, Rukwa, Songwe na Mbeya uliofanyika katika ukumbi wa Zuri home ground mkoani hapa ambapo amewataka wajumbe wa bodi hizo kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na katiba iliyowekwa ili kupunguza migogoro.
Awali akitoa taarifa ya lengo la mkutano huo Kabidhi Wasii mkuu na afisa mtendaji mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi amesema kuwa bodi bado zinakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wajumbe wa bodi za wadhamini kuwa na uelewa mdogo wa wajibu na sheria za bodi hizo.
Aidha amesema kuwa jumla ya bodi 646 zimesajiliwa katika mikoa sita iliyoshiriki mkutano huo ambapo mkoa wa Katavi umesajili bodi za wadhamini 07, Kigoma 56, Tabora 65, Mbeya 174, Rukwa 20 na Songwe 327.