Mpanda FM
Mpanda FM
12 February 2026, 1:36 pm

Anyulumye Longo Afisa Ustawi manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi. Picha na Anna Mhina
Wazazi na walezi katika manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, wamesema kuwa uelewa mdogo wa jamii juu ya umuhimu wa elimu na hali ya umasikini vinachangia mtoto kutokupelekwa shule
Na Anna Mhina
Uelewa mdogo wa umuhimu wa elimu kwa watoto na hali duni ya maisha imetajwa kuwa chanzo cha baadhi ya wazazi na walezi kutowapeleka watoto wao shule.
Wakizungumza na Mpanda radio FM baadhi ya wazazi na walezi katika manispaa ya Mpanda wamesema kuwa jamii bado ina uelewa mdogo wa umuhimu wa elimu kwa watoto huku wengine wakieleza hali ya umasikini inavyochangia mtoto kutopelekwa shule.
Anyulumye Longo, Afisa Ustawi manispaa ya Mpanda ameeleza umuhimu wa elimu kwa watoto mbali na kuwaongezea ujuzi na maarifa pia elimu humsaidia mtoto kutimiza ndoto zake pamoja na kumuwezesha kupata fursa mbalimbali za ajira.
Ikumbukwe kuwa January 27, 2026 mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusufu aliwaagiza viongozi ngazi ya mitaa na kata kupita nyumba kwa nyumba ili kuwasaka watoto ambao hawajaripoti shule.