Mpanda FM

34 wadakwa kwa makosa mbalimbali Katavi

6 February 2026, 3:19 pm

SACP Kaster Ngonyani kamanda wa polisi Katavi. Picha na Anna Mhina

“Tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 34 kwa makosa mbalimbali”

Na Anna Mhina

Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limeendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa raia na mali zao kwa kufanya operasheni, doria na misako kwa lengo la kuzuia uhalifu na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 34 kwa makosa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amesema kuwa kwa kipindi cha mwenzi January 2026 wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 34 ambapo kati yao watuhumiwa watatu wamekamatwa wakiwa na nyara za serikali huku watuhumiwa tisa wakiwa na silaha haramu.

Sauti ya kamanda

Katika hatua nyingine Ngonyani amesema kuwa watuhumia watatu wamekamatwa wakiwa na noti  bandia kumi za dola mia moja huku wengine wawili wakiwa na ng’ombe kumi mali ya Hassan Ndege walizoiba January 27, 2026 kwa kuvunja zizi.

Sauti ya kamanda

Hata hivyo jeshi la polisi mkoa wa Katavi limetoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo viovu vya uhalifu.