Mpanda FM
Mpanda FM
5 February 2026, 3:59 pm

Baraka Nkondo daktari bingwa wa magonjwa ya pua, koo na masikio. Picha na Leah Kamala
“Magonjwa haya yanapotokea na jumuisha na magonjwa ya kuambukiza”
Na Leah Kamala
Wananchi manispaa ya mpanda mkoani Katavi wameshauriwa kujenga desturi ya kupima afya zao mara kwa mara na kufuata ushauri wa daktari wanapopata matatizo yanayohusiana na pua, koo na masikio badala ya kujitibu wenyewe.
Akizungumza na Mpanda redio FM daktari bingwa wa magonjwa ya pua, koo na masikio kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa katavi daktari Baraka Nkondo amesema kuwa kufuata ushauri wa daktari ikiwemo kutumia dawa kwa usahihi na kukamilisha dozi ni hatua muhimu katika kupona na kuzuia kurejea kwa magonjwa hayo.
Nao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuongezewa wataalamu mbalimbali ili waweze kupewa elimu kuhusiana na magonjwa hayo.
Wananchi wanahimizwa kujenga utamaduni wa kutafuta huduma za kitaalamu kama kupima mapema kufuata ushauri wa daktari na kuepuka matumizi holela ya dawa ili kulinda afya zao na kuzuia athari za muda mrefu.