Mpanda FM

Mume ang’atwa mdomo kisa mchepuko

4 February 2026, 9:21 am

Baada ya kupatiwa matibabu. Picha na Anna Mhina

“Niligongewa mlango saa tano za usiku “

Na Anna Mhina

Kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30-35 mkazi wa mtaa wa Mpadeko uliopo kata ya Makanyagio manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amenusurika kukatwa nyama ya mdomo baada ya kung’atwa na mke wake.

Akizungumza na Mpanda redio FM kijana huyo ameeleza chanzo kilichopelekea mke wake kufanya tukio hilo ikiwa ni wivu wa mapenzi baada yakupokea simu iliyopigwa na mwanamke mwingine.

Sauti ya mhanga

Ivo Chambala ni mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeko uliopo kata ya Makanyagio amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza namna alivyolitatua kwa kuanza kumpeleka kijana hospitali ili kuweza kupatiwa matibabu.

Sauti ya mwenyekiti

Kwa upande  wake Sajent Veronica Goy kutoka kitengo cha  dawati la jinsia na watoto Mpanda amewataka wanaume kuacha tabia ya kuogopa kuripoti vitendo vya kikatili wanayofanyiwa na wenza wao ili kupunguza vitendo hivyo.

Sauti ya sajent Veronica

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo amesema hili ni tukio la tatu kwa wanaume kufanyiwa ukatili na wake zao na kukaa kimya ambapo January 2026 mwanaume mmoja alifanyiwa ukatili kwa  kupigwa na kigoda kichwani