Mpanda FM

Wafanyabiashara Katavi kunufaika na IDRAS

29 January 2026, 5:00 pm

Wafanyabiashara wakiwa kwenye mafunzo. Picha na Betord Chove

“Mfumo huu utatusaidia namna ya ulipaji kodi”

Na Betord Chove

Wafanyabiashara mkoani Katavi wameeleza kufurahishwa na elimu iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Katavi kuhusu mfumo mpya wa uwasilishaji na ulipaji wa kodi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Wakizungumza mara baada ya kutamatika kwa mafunzo hayo wamesema kuwa elimu hiyo imewasaidia kuuelewa vizuri mfumo huo na kurahisisha kulipa kodi kwa wakati, pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kikodi jambo linalotarajiwa kuchochea ukuaji wa biashara na kuimarisha ushirikiano kati ya TRA na walipakodi.

Sauti za wafanyabiashara

Kwa upande wake Joshua Mille meneja msaidizi wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA  mkoa wa Katavi akizungumzia kuhusu mfumo huo wa IDRAS, amesema mfumo huo utakuwa suluhisho la  changamoto zilizokuwa zinajitokeza baina ya wateja na mamlaka.

Sauti ya meneja

 Mfumo huo wa IDRAS utaanza kufanya kazi February 09 mwaka 2026.