Mpanda FM
Mpanda FM
29 January 2026, 4:51 pm

Jamila Yusuph mkuu wa wilaya ya Mpanda. Picha na Anna Mhina
“Tumeshatoa hamasa sasa ni muda wa kuchukua hatua kwa wazazi”
Na Anna Mhina
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewaagiza wenyeviti na watendaji wa mitaa pamoja na viongozi wa kata wakiwemo maafisa tarafa kupita nyumba kwa nyumba kuwasaka watoto ambao hawajaripoti shule.
Jamila ametoa agizo hilo kufuatia watoto wengi kutoripoti shule kwa wakati ambapo mpaka sasa hivi wanafunzi wa darasa ya awali, shule ya msingi na sekondari ambao wameripoti hawajafikia asilimia 70.
Katika hatua nyingine Jamila amesema kuwa wao kama serikali wameshatoa hamasa kwa jamii sasa ni muda wakuchukua hatua kwa mzazi ambaye anazembea kumpeleka mtoto wake shule huku akipiga marufuku mtoto kukataliwa kwasababu ya michango.
Jamila ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika zoezi la upandaji miti lililofanyika January 27, 2026 ikiwa ni kumbukizi ya mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia suluhu Hassan.