Mpanda FM
Mpanda FM
27 January 2026, 9:07 pm

“Amewataka wananchi waliopewa miti kwenda kuipanda na kuitunza ili kusaidia upatikanaji wa hewa safi pamoja na kulinda mazingira.“
Na Samwel Mbugi-Katavi
Wananchi wa wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wameungana na serikali kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kupanda miti katika eneo la shule ya msingi songambele.
Akizungumza na wananchi waliofika katika ziara hiyo mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoka amewataka wananchi waliopewa miti kwenda kuipanda na kuitunza ili kusaidia upatikanaji wa hewa safi pamoja na kulinda mazingira.
Awali akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Benard Ntiliyo amesema kuwa halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira kwa pamoja, wamesambaza miche ya miti 339,534 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kupitia ziara hiyo mkuu wa mkoa wa Katavi amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto waliofikia umri wa kuandikishwa kwenda shule wameandikishwa ili kuwatendea haki ili wapate haki yao ya msingi ya elimu.