Mpanda FM
Mpanda FM
27 January 2026, 12:51 pm

“Unywaji wa pombe kupitiliza husababisha mtu kupata vidonda vya tumbo”
Na Anna Mhina
Ukosefu wa elimu ya afya ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo imetajwa kuwa sababu ya kuongezeka kwa ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi na kueleza kuwa hawana uelewa kuhusiana na ugonjwa huo hali iliyopelekea kuiomba mamlaka husika kutoa elimu kwa jamii.
Mstafa Kombo ni daktari katika hospital ya manispaa Mpanda ameeleza sababu zinazopelekea mtu kupata ugonjwa huo wa vidonda vya tumbo ikiwa ni pamoja na unywaji pombe kupitiliza, uvutaji wa sigara sambamba na ulaji wa vyakula vyenye uchachu.
Aidha Kombo ameeleza dalili za ugonjwa huo na kuiasa jamii kuchukua tahadhari pindi wanapoona hali hiyo kwa kuwahi kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.