Mpanda FM
Mpanda FM
27 January 2026, 12:43 pm

Kushoto ni Abigael Hendry Leina Katibu wa mbunge wa Mpanda mjini. Picha na John Benjamin
“Malengo ya mheshimiwa mbunge sio kuwapa mafunzo tuu”
Na John Benjamin
Viongozi wa makundi mbalimbali ya vijana yakiwemo bodaboda, machinga, wachimbaji wadogo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamepatiwa elimu ya matumizi sahihi ya fedha.
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Haidary Hemed Sumry ameandaa mafunzo hayo ambapo katibu wa mbunge huyo Abigael Hendry Leina amesema kuwa katika kipindi cha kampeni walibaini kuwepo kwa changamoto ya vijana kukosa mitaji hivyo kupitia mafunzo hayo yanakwenda kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa makundi ya vijana waliohudhuria katika mafunzo hayo wamemshukuru mbunge ambapo wamesema kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuwanufainisha katika shughuli zao za kujitafutia kipato.
Maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa kwa mwaka 2026 yameanza Januari 19, 2026 katika viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga ambapo maadhimisho hayo yameandaliwa na serikali kupitia wizara ya fedha kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya fedha ikiwemo matumizi sahihi ya huduma za kifedha.