Mpanda FM

Ujenzi kituo cha afya Ibindi kicheko kwa wananchi

26 January 2026, 10:06 am

Ujenzi wa kituo cha afya Ibindi ukiendelea. Picha na Samwel Mbugi

“Kwa muda mrefu tumehangaika lakini kwa bahati nzuri mradi umetufikia”

Na Samwel Mbugi

Wananchi wa kata ya Ibindi wameishukuru serikali kwa kuwapelekea mradi wa kituo cha afya Ibindi ambacho wamesema kikikamilika kitakwenda kuondoa changamoto ya kusafiri umbali mrefu.

Wakizungumza katika ziara ya kamati ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa katavi wemeipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kuwasogezea huduma za afya kwa ukaribu zaidi.

Sauti za wananchi

Mwenyekiti wa hama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa katavi Iddi Kimanta kwa niaba ya kamati ya siasa mkoa wa katavi ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kituo cha afya na kuitaka serikali kusimamia mradi huo kukamilika kwa haraka.

Sauti ya Kimanta

Hata hivyo mwenyekiti amempongeza diwani wa kata ya Ibindi Mdakuni Matongo kwa juhudi zake binafsi kupeleka maji kati mradi hio unaoendelea kujengwa.

Sauti ya Kimanta