Mpanda FM
Mpanda FM
24 January 2026, 1:21 pm

“Maji tunayokunywa ni machafu tunaumwa matumbo”
Na Restuta Nyondo
Baadhi ya wananchi katika kitogoji cha Ivungwe C Kijiji cha Manga manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia kutumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya shughuli za kimaendeleo.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM wamesema kuwa kipindi hiki cha masika wanategemea maji yanayotiririka kutoka mlimani huku kipindi cha kiangazi huwalazimu kwenda umbali mrefu kufuata maji licha ya maji hayo kutokuwa safi na salama hali inayosababisha kuugua magonjwa ya matumbo.
Diwani wa kata ya Kasokola Filibert Ibumi amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa wananchi ambapo ameiomba serikali kuhakikisha wanafikisha huduma hiyo kwa uharaka zaidi ili kunusuru changamoto wanazozipata wananchi hao.
Mkurungezi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira manispaa ya Mpanda MUWASA Rehema Nelson amesema kuwa upo mpango ambayo unakwenda kufanyika kupitia mradi wa bwawa la Milala ambayo inakwenda kusaidia kuondoa chngamoto ya maji katika eneo hilo.
Kitongoji cha Ivungwe C kilichopo kijiji cha Manga kata ya Kasokola chenye kaya 35 kinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji hali inayosababisha kutumia maji na wanyama.