Mpanda FM
Mpanda FM
22 January 2026, 5:11 pm

Kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Picha na Samwwel Mbugi
“Tumekuja hapa tumeambiwa hakuna maji hatukubaliani na hiki kitu”
Na Samwel Mbugi
Kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Katavi ikiongozwa na mwenyekiti wa chama Iddi Kimanta imeendelea na ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM Katika halmashauri ya Nsimbo.
Wajumbe wa kamati ya siasa wakizungumza katika ziara hiyo wameutaka uongozi wa hospitali ya halmashauri ya Nsimbo kuhakikisha wanaweka mazingira katika hali ya usafi na wezeshi kwa wagonjwa kupata huduma bila kukutana na changamoto.
Awali akisoma tarifa kwa kamati ya siasa katibu wa afya (DHS) halmashauri ya Nsimbo Lucas Joseph Mrope amesema pamoja na kutoa huduma za kijamii pia wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa watumishi kwa 75% pamoja na ukosefu wa gari la wagonjwa.
Hata hivyo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Katavi Iddi Kimanta amemtaka mkuu wa mkoa kuhakikisha hospital ya halmashari inapata maji na umeme haraka iwezekanavyo ili wagonjwa kuondokana na adha wanayokutana nayo wakati wa mahitaji muhimu.