Mpanda FM
Mpanda FM
21 January 2026, 7:24 pm

“Ndugu zangu najua ninyi ni wafugaji na mnaingia gharama kubwa za madawa”
Na Benny Gadau
Diwani wa kata ya Ibindi halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mdakuni Matongo amewasihi wafugaji kushirikiana kukamilisha ujenzi wa josho la mifugo.
Amezungumza hayo katika kikao cha kusikiliza kero za wafugaji kilichofanyika Kijiji cha Muungano, huku akichangia kiasi cha shilingi laki nne kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa josho la mifugo, akibainisha kuwa mradi huo utakuwa msaada kwa wafugaji pamoja na kuboresha ustawi wa mifugo yao.
Aidha baadhi ya wafugaji wametoa shukrani zao kwa diwani huyo kwa kutoa kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa josho la mifugo, huku wakiahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.
Kukamilika kwa ujenzi wa josho hilo kunatajwa kuwa msaada mkubwa kwa wafugaji wa Kata ya Ibindi pamoja na baadhi ya kata jirani zikiwemo Itenka na Stalike katika Halmashauri ya Nsimbo, Mkoa wa Katavi.