Mpanda FM

Epukeni vitambi kwa kuzingatia ulaji

20 January 2026, 6:39 pm

Neema Kambi  afisa lishe manispaa ya Mpanda. Picha na Samwel Mbugi

“Sababu ya kwanza ni ulaji wa chips”

Na Samwel Mbugi

Ulaji usiofaa watajwa kuwa chanzo cha ongezeko la vitambi kwa baadhi ya  wanaume na wanawake mkoani Katavi.

 Akizungumza na mpanda radio FM afisa lishe manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Neema Kambi  amesema miongoni mwa sababu zinazosababisha kitambi kwa wanawake na wanaume ni vyakula vya haraka ikiwemo chips na nyama choma.

Sauti ya afisa lishe

Neema ameitaka jamii  kubadilika kutokana na ongezeko la  magojwa yasiyo ya kuambukiza yanayotokana na ulaji usiofuata makundi yote sita ya chakula kama vile kisukari.

Sauti ya afisa lishe

Katika miongo michache ya nyuma hapa nchini Tanzania na baadhi ya nchi duniani baadhi ya watu kutokana na ukosefu wa elimu walivitazama vitambi kama dalili ya ustawi mzuri wa maisha.