Mpanda FM
Mpanda FM
19 January 2026, 6:43 pm

“Mfano kwenye kijiji hiki cha Kasokola kisima kipo kimoja tena cha mtu binafsi”
Na Restuta Nyondo
Wananchi wa kijiji cha Kasokola halmashauri ya manispaa ya Mpanda wameiomba serikali kuchukua hatua za uwezeshaji miundombinu ya maji ili kuboresha kilimo cha umwagiliaji.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wamesema kuwa wanapata changamoto ya kufanya kilimo hicho kutokana na kutokuwepo kwa maeneo wezeshi ya kilimo cha umwagiliaji kama bustani kwani hakuna visima wala mabwawa katika kijiji hicho.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Melack Simon amesema wamekua wakifanya jitihada mbalimbali za upatikanaji maji kupitia Muwasa lakini bado maji hayo hayakidhi mahitaji kuwezesha kilimo cha umwagiliaji.
Kwa upande wake afisa kilimo kata ya Kasokola Benatus Ngoda amesema kuwa kilimo cha umwagiliaji ni fursa na rafiki wa mazingira hasa katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.
Kutokana na kuendelea kuwepo kwa mabadiliko ya tabianchi kilimo cha umwagiliaji kinatajwa kama njia bora katika upatikanaji wa chakula misimu yote .