Mpanda FM
Mpanda FM
15 January 2026, 3:36 pm

“Tunaomba daktari atuelimishe kuhusu huu ugonjwa”
Na Samwel Mbugi
Kutokana na uwepo wa ugonjwa wa kifafa cha mimba katika jamii wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wameiomba serikali kutoa elimu itakayosaidia kufahamu na kuelewa dalili na sababu zinazosababisha.
Wameyasema hayo wakizungumza na Mpanda Radio FM ambapo wameiomba serikali kutoa elimu itakayosaidia kufahamu ugonjwa huo inasababishwa na nini pamoja na viashiria vya kupata kifafa cha mimba.
Kwa upande wake Dr. Mundhiri Bashiri kutoka hospital ya manispaa ya wilaya ya Mpanda amesema ugonjwa huo anaweza kumpata mama mjamzito na dalili za kifafa cha mimba ni mgonjwa kuonyesha dalili za degedege.
Hata hivyo Dr. Mundhiri amesema ugonjwa huo huwa unasababishwa na kondo la nyuma la mtoto likipata shida wakati wa kujitengeneza.
Ugonjwa wa kifafa cha mimba ni miongoni mwa magonjwa hatari sana kwa maisha ya wanawake wengi wajawazito nchini Tanzania.