Mpanda FM
Mpanda FM
15 January 2026, 2:55 pm

Uongozi wa shule ya msingi Mpanda pamoja na mwenyekiti wa mtaa. Picha na Roda Elias
“Tumeridhisha na ujenzi wa choo”
Na Roda Elias
Serikali ya mtaa wa Mpanda hotel manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imeridhishwa na ujenzi wa mradi wa matundu ya choo cha wasichana unaoendelea katika shule ya msingi Mpanda.
Akizungumza katika ukaguzi wa mradi huo uliofanyika katika shule ya msingi Mpanda mwenyekiti wa mtaa huo Ibrahim Msanda amempongeza mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa kusimamia ujenzi wa choo hicho.

Choo cha wasichana katik shule ya msingi Mpanda
Kwa upande wao wazee wa baraza la mtaa huo wakiongozwa na mzee Robert Mgangala wameupongeza uongozi wa shule hiyo huku wakiomba kupatikana kwa ufumbuzi juu ya changamoto Mbalimbali zinazoikumba shule hiyo.
Akitoa taarifa ya mradi huo mwalimu mkuu wa shule hiyo Khadija Chikawe amesema kuwa wamepitia changamoto kutoka kwa mzabuni ambapo mpaka sasa wamepata ufumbuzi wa changamoto hiyo.
Mradi wa ujenzi wa choo cha wasichana katika shule hiyo ni mradi ambao umejengwa na serikali na mapato ya ndani ya halmashauri na vyoo hivi vina matundu saba moja likiwa ni tundu kwa ajiri ya wanafunzi walio na mahitaji maalumu.