Mpanda FM

Wananchi Mpanda walia na MACPANDO

13 January 2026, 3:17 pm

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akitoa maelekezo kwa kamati. Picha na Samwel Mbugi

“Mnisikilize vizuri huyuhuyu MACPANDO lazima afike mwisho”

Na Samwel Mbugi

Wananchi wa mtaa wa Tulieni kata ya Nsemlwa wamelalamikia migogoro ya viwanja inayotokana na kampuni ya MACPANDO iliyopewa tenda ya usanifu wa ramani za viwanja katika mtaa huo.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa Wilaya Jamila Yusuph wamesema ni muda mrefu umepita hawajakabidhiwa viwanja na kumekuwa kukijitokeza migogoro  inayotokana na uuzaji wa viwanja kinyume na utaratibu unaotakiwa kufuatwa.

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa kamati ya upimaji wa viwanja Salum Moshi Kakoko amesema kampuni ya MACPANDO imeshindwa kutekeleza mkataba waliokubaliana na wananchi jambo hilo limekuwa likuwa likichangiwa na vingozi wa serikali kuvuja kamati kwa masilahi ya kampuni.

Sauti ya mwenyekiti

Aidha diwani wa kata ya Nsemlwa Alex Ngerenza amesema kuwa changamoto kubwa inasababishwa na Kamati ya upimaji wa viwanja kwa kuuza viwanja vya wananchi kinyume na utaratibu.

Sauti ya diwani

Kwa upande wa kampuni ya Macpando ikiwakilishwa na Masudi Saidi amesema changamoto kubwa inayojitokeza ni baadhi ya wananchi waliopimiwa viwanja kuto kufuata utaratibu wa mkataba kama walivyokubaliana.

Sauti ya mwakilishi wa kampuni

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph mara baada ya kusikiliza pande zote mbili ametoa siku saba Kwa kamati kufika eneo husika na kutatua changamoto zote ili kila mtu apate haki yake.

Sauti ya mkuu wa wilaya

Jamila ameshauri katika makubaliano ambayo watakubalianana inatakiwa mwananasheria wa halmashari kuwepo ili kushauli maswala ya kisheria katika makubaliano hayo ya mkataba.