Mpanda FM
Mpanda FM
12 January 2026, 9:28 am

“Mwamko wa elimu bado ni mdogo kwa mkoa wa Katavi”
Na Anna Mhina
Kutokuwa na mwamko wa elimu kumetajwa kama sababu inayopelekea wazazi kuwa na mwamko mdogo katika zoezi la uandikishaji kwa watoto mapema.
Wakizungumza na Mpanda radio FM baadhi ya wazazi na walezi wameeleza kuwa ukosefu wa elimu husababisha wazazi wengi kutokutoa kipaumbele cha kuwaandikisha shule watoto na kuwajali kwenye masuala ya sikukuu.
Kwa upande wake afisa elimu wa elimu ya awali na msingi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Johari Mwasha ameeleza namna ambavyo zoezi la uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza linavyoendelea sambamba na kueleza matarajio yao ikiwa ni kufikia asilimia 75 ifikipo January 13, 2026.
Katika hatua nyingine Mwasha amewataka wazazi na walezi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda wasiache kuwaandikisha watoto kwa kisingizio cha kukosa cheti cha kuzaliwa.
Ikumbukwe kuwa zoezi la uandikishwaji wa wanafunzi kujiunga na darasa la awali pamoja na darasa la kwanza kwa Mpanda lilianza rasmi October 2025 ambapo wanafunzi hao wanatarajiwa kuanza masomo yao ifikapo January 13, 2026.