Mpanda FM

Watoto wawili kutoka mazingira hatarishi hadi malezi salama

7 January 2026, 10:25 am

Mama akiwa na watoto wake wawili nyakati za usiku akitafuta mahali pa kulala. Picha Anna Milanzi

“Watoto hao walikuwa wanaishi katika mazingira hatarishi”

Na Anna Milanzi

Makala hii inaangazia safari ya miezi tisa ya ufuatiliaji wa kijamii kuhusu watoto wawili waliokuwa wakiishi katika mazingira hatarishi. Kupitia ushirikiano wa jamii, viongozi wa eneo husika, na mamlaka za ustawi wa jamii, hatua zilichukuliwa hadi serikali ikawachukua watoto hao na kuwaweka katika malezi salama.
Makala hii inalenga kuonesha umuhimu wa ulinzi wa mtoto, uwajibikaji wa jamii, na mshikamano kati ya wananchi na taasisi za umma. Ili kulinda maslahi na haki za watoto. Majina, maeneo mahususi, na taarifa zinazoweza kuwatambulisha hazijatolewa kwa kuzingatia haki na ulinzi wa mtoto.