Mpanda FM
Mpanda FM
24 December 2025, 1:17 pm

Baadhi ya vijana wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkuu wa wilaya Mpanda. Picha na Samwel Mbugi
“Wilaya yetu ya Mpanda tumeshapokea billion 24”
Na Samwel Mbugi
Vijana wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi wameshirikiki kongamano lililowakutanisha na mkuu wa wilaya Jamila Yusuph kwajili ya kufahamishana fursa zinazopatikana ndani ya wilaya ambazo wanapaswa kunufaika nazo.
Akizungumza na vijana waliohitimu shule ya msingi, sekondari, vyuo na vyuo vikuu kutoka makundi mbalimbali yaliyofika ukumbi wa manispaa mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema wilaya ya mpanda imepokea billion 24 kwajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya wilaya.
Pia Jamila amesema mpaka sasa takwimu zilizokusanywa kwaajili ya kubaini idadi ya vijana waliopo wilaya ya mpanda mpaka sasa imefikia elfu tatu wakiwa na elimu tofauti tofauti kuanzia ngazi ya darasa la saba mpaka vyuo vikuu.
Kwa upande wa baadhi ya vijana waliohudhuria kongamano hilo wametoa maoni yao na ushauri mseto namna ya kupata fursa zinazopatikana ndani ya wilaya ya mpanda.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani ameanzisha wizara ya vijana itakayokuwa inashughulikia changamoto mbalimbali za vijana.