Mpanda FM

TAG Katavi yaeleza umuhimu wa kuwalea wazazi wa kiroho

24 December 2025, 12:53 pm

Kanisa la TAG Living Water wakiwa kwenye ibada ya kumtegemeza mchungaji. Picha na Anna Mhina

“Mchungaji anatakiwa apate muda wa kumtafuta Mungu”

Na Anna Mhina

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)  Living Water lililopo mtaa wa Kwalakwacha kata ya Nsemulwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi December 21, 2025 limeazimisha sherehe za kumtegemeza mchungaji ikiwa ni moja kati ya mpango wa kitaifa wa dhehebu hilo.

Akizungumza na Mpanda radio FM mzee wa kanisa hilo Edison Danford ameeleza lengo la mpango huo ni kuwawezesha wachungaji kupata muda wa kumtafuta Mungu ili waweze kuandaa mafundisho sahihi sambamba na kueleza zawadi walizozitoa ikiwa ni pamoja na vyakula.

Sauti ya mzee wa kanisa

Aidha baadhi ya waumini wa kanisa la Living Water akiwemo Reuben Kateba na Sara Petro wamefurahishwa na uwepo wa mpango huo wa kuwategemeza wachungaji na kusema kuwa ni muhimu kuwajali kwani ni agizo la Mungu.

Sauti za waumini

Rocky Petro ni mchungaji wa kanisa hilo amewashukuru waumini kwa kujitoa kwao na kuahidi kuendelea kuwaombea huku mama mchungaji Agatha Rocky akiwapongeza kwa kuonesha upendo wao kwa Mungu.

Sauti ya baba na mama mchungaji

Zoezi hilo la kuwategemeza wachungaji kwa dhehebu la TAG kitaifa hufanyika kila mwisho wa mwaka ambapo kwa mwaka huu baadhi ya makanisa yamefanya zoezi hilo December 7.