Mpanda FM

Mwanaume afa maji kwenye dimbwi la kufyatulia tofali Katavi

20 December 2025, 4:50 pm

Jeshi la zimamoto na uokoaji likiwa limebeba mwili wa mwanaume huyo. Picha na Anna Mhina

“Kumekuwa kama dampo la watu kufia huku”

Na Anna Mhina

Mtu mmoja jinsia ya kiume ambaye hajafahamika jina lake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40-45 amekutwa amefariki dunia ndani ya dimbwi la maji mtaa wa Mpanda hotel viwandani uliopo kata ya Mpanda hotel mkoani Katavi.

Akizungumza na Mpanda radio FM  mkuu wa kitengo cha operesheni zimamoto na uokoaji Katavi Sajent Emmanuel Ruta amesema December 20, 2025 majira ya saa tatu asubuhi walipokea taarifa za uwepo wa mwili huo ndani ya dimbwi la maji na kuwataka wananchi kuchukua tahadhali hususani kipindi hiki cha mvua.

Sauti ya Sajent Ruta

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda hotel Ibrahimu Mzanda ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo na hatua alizozichukua pamoja na kuwatoa hofu wananchi ili waweze  kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.

Sauti ya mwenyekiti

Nao baadhi ya majirani wameonesha kusikitishwa na tukio hili na kuingiwa na hofu kwa kusema kuwa imekuwa desturi ya eneo hilo kuwa dampo la kukutwa miili ya watu.

Sauti za majirani

Tukio hili limetokea ikiwa ni siku chache zimepita ambapo December 17, 2025 mtaa wa Migazini uliopo kata ya Nsemulwa kuliokotwa mwili wa mtu ambaye hakujulikana.